Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres alaani shambulio huko Afghanistani

Guterres alaani shambulio huko Afghanistani

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani shambulio lililofanywa hii leo huko Kabul, Afghanistani.

Tukio hilo katika jengo la mahakama kuu lilisababishwa na mtu aliyejilipua nje ya jengo hilo na kusababisha vifo na majeruhi.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric akizungumza na waandishi wa habari amemnukuu Katibu mkuu Guterres akisema kuwa mashambulizi ya kiholela dhidi ya raia na wafanyakazi wa taasisi za mahakama ni ukiukaji wa haki za binadamu na sheria za kimataifa.

Amesema kitendo hicho hakiwezi kuhalalishwa kwa misingi yoyote ile.

Bwana Guterres ametuma salamu za rambi rambi kwa wafiwa, wananchi wa Afghanistan na serikali yao.

Ametaka wahusika wa shambulio hilo la leo na wafikishwe mbele ya sheria.

Photo Credit
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres.(Picha:UM/Jean-Marc Ferré/maktaba)