Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulio la jengo la Al-Janoub si ishara nzuri

Shambulio la jengo la Al-Janoub si ishara nzuri

Pakua

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed amelaani vikali shambulio katika jengo la kamati ya kuratibu sitisho la chuki huko Dhahran Al-Janoub, Yemen.

Bwana Ahmed amesema ni jambo la kusikitisha mno kuwa mashambulizi hayo yamefanyika wakati ambapo tumetoa wito wa marejesho ya hali ya kutokuwepo kwa uhasama, na jengo hilo lilitarajiwa kutumiwa na kamati itakayosimamia wito huo na kuripoti ukiukwaji wowote.

Vile vile amesema Umoja wa Mataifa hutumia jengo hilo kuendesha shughuli zake na tukio hili si ishara ya nia njema.

Mjumbe huyo amewasihi kikundi cha Ansal Allah na Bunge la Wananchi kukubali kushiriki katika warsha ya kamati ya sitisho la chuki, akisisitiza umuhimu wa kuunga mkono kazi ya kamati hiyo ambayo ni muhimu kwa ajili ya mafanikio katika sitisho la chuki mpya.

Amesema ni kwa maslahi ya pande zote mbili katika mgogoro kuanza haraka kutekeleza utaratibu wa sitisho la chuki yenye kudumu katika siku na wiki zijazo kwa ajili ya kufungua fursa mpya ya mazungumzo.

Photo Credit