Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko kwa wanawake na wasichana:Puri

Kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko kwa wanawake na wasichana:Puri

Pakua

Kongamano la wadau mbalimbali kuhusu “uwezeshaji wa wanawake kiuchumi katika mabadiliko ya ulimwengu wa kazi” linafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hii leo.

Washiriki kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, mashirika ya Umoja wa Mataifa, asasi za kiraia na wadau wengine wa masuala ya wanawake wanajadili mada hiyo ambayo itakuwa kauli mbiu ya kikao cha 61 cha kamisheni ya hali ya wanawake (CSW-61) kitakachoanza mwezi machi mwaka huu.

Akimwakilisha mkurugenzi mkuu wa kitengo cha Umoja wa mataifa cha masuala ya wanawake UN Women, naibu mkurugenzi mtendaji wa UN Women Bi Lakshmi Puri amesema

(SAUTI YA PURI)

“Tunaamini kwamba pamoja tutaweza kupiga hatua kubwa kwa wanawake na wasichana wote. Tuko katika wakati muhimu wa kufikia usawa wa kijinsia na haki za binadamu za wanawake na ajenda ya 2030 ambayo inatoa kipaumbele kwa kufikia sio tu kuchagiza usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana kama lengo la maendeleo endelevu namba 5, bali sasa ni utekelezaji, vipi tunafuatilia na kuangalia utekelezaji”

Ameongeza kuwa wanawake ni muhimu sana katika kufikia ajenda ya 2030

(SAUTI YA PURI)

“Haki sawa za kiuchumi kwa wanawake, uwezeshaji wa kiuchumi na uhuru ni muhimu katika kufikia ajenda ya 2030. Zaidi ya hayo fursa sawa kwa wanawake, kwa ajira na uzalishaji kamilifu na kazi zenye hadhi na malipo sawa kwa kazi sawa ni changamoto kubwa katika ujumuishwaji kikamilifu wa wanawake katika uchumi rasmi."

Photo Credit
Naibu mkurugenzi mtendaji wa UN Women Bi Lakshmi Puri.(Picha:UM/Rick Bajornas)