Skip to main content

Jukumu la dini katika kuleta amani na kuzuia migogoro ni kubwa: Dieng

Jukumu la dini katika kuleta amani na kuzuia migogoro ni kubwa: Dieng

Pakua

Jukumu muhimu la kuleta amani ya kudumu na kuzuia migogoro, ukatili wa itikadi kali na uhalifu wa kupindukia ni la kila nchi. Hayo yamesemwa na mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari Adama Dieng alipozungumza kwenye kongamano kuhusu jukumu la dini na mashirika ya Imani katika masuala ya kimataifa .

Katika kongamano hilo kwenye Umoja wa mataifa Jumatatu Dieng ameongeza kuwa nchi na viongozi wa dini ni lazima wachagize mila za kukumbatia tamadunia na Imani mbalimbali katika njia iliyo bora.

(DIENG CUT 1)

“Wana jukumu la kulinda haki za binadamu za watu wao kwa usawa bila ubaguzi, hata hivyo jumuiya ya kimataifa ikiwemo mashirika ya kikanda, Umoja wa Mataifa na asasi za kiraia lazima wawe tayari kuziunga mkono nchi hizo”

Kwa muktada huu ametoa msisitizo wa jukumu la wawakilishi wa dini na mashirika mbalibali ya Imani tofauti.

(DIENG CUT 2)

“Viongozi wa dini wana jukumu muhimu , na wawo pamoja na mashirika ya Imani na dini mbalimbali wana wajibu wa kuchangia katika ujenzi wa jamii zenye amani, jumuishi na imara ambazo zinaweza kukabili migogoro, ukatili wa itikadi kali na uhalifu wa kimbari. Wanaweza kufikia na kushawishi idadi kubwa ya watu, kutoa msaada wakati wa dharura, kukidhi mahitaji ya jamii zilizotengwa na pia kushughulikia malalamiko kama yanavyoibuka na kuchagiza haki za jamii zao”

Amehimiza kuwa viongozi hao wa dini ni wapatanishi wa mashinani na wanahitaji msaada na uungwaji mkono wa jumuiya ya kimataifa katika shughuli zao za kila siku za kuchagiza amani.

Photo Credit
UN Photo - Jean-Marc Ferre