Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kimataifa kuhusu historia ya Afrika waanza leo Havana, Cuba

Mkutano wa kimataifa kuhusu historia ya Afrika waanza leo Havana, Cuba

Pakua

Kamati ya kimataifa ya kisayansi kuhusu historia ya Afrika inafanya mkutano wake wa tano ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO mjini Havana, Cuba kuanza leo Jumatatu Januari 23 hadi Januari 28.

Lengo kuu la mkutano huo ni kufanya tathmini ya maendeleo ya kazi na kuhalalisha makaratasi yaliyowasilishwa na waandishi na kujadili mifumo ya kuikamilisha mwakani.

Mkutano huu pia utawapa fursa wanachama wa kamati hiyo kubadilishana uzoefu na watafiti wa Cuba, wasanii, vyama vya kiraia na waandishi wa habari kuhusu mbinu mpya na dhana ya maendeleo kwa ajili ya maandalizi ya ukurasa mpya wa kihistoria.

Kama sehemu ya mkutano huu, tamasha la Ray Lema na wanamuziki wa Cuba limeandaliwa ili kuzindua Umoja wa Wasanii kwa ajili ya historia ya Africa nchini Cuba.

Photo Credit
(Picha:UM/Milton Grant)