Kampeni ya kupinga chuki dhidi ya Waislamu yaleta nuru
Pakua
Juma hili, katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kulifanyika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu chuki na ubaguzi dhidi ya uislamu na waislamu.
Mkutano huo wa siku moja uliandaliwa kwa pamoja na ofisi za ubalozi za Canada na Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, ujumbe wa Muungano wa Ulaya na Umoja wa nchi za kiislamu duniani, OIC.
Wakati wa mkutano huo uliolenga kuchambua madhila yanayokumba waislamu duniani, Umoja wa Mataifa ulizindua kampeni iitwayo Pamoja yenye lengo la kukabiliana na chuki na ubaguzi dhidi ya uislamu na waislamu duniani. Je nini kilijiri? Na ni mapendekezo yapi yalitolewa? Tuungane basi na Flora Nducha kwa uchambuzi zaidi.