Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takwimu bora kuhusu jinsia ni muhimu kwa SDG's:UN Women

Takwimu bora kuhusu jinsia ni muhimu kwa SDG's:UN Women

Pakua

[caption id="attachment_306809" align="aligncenter" width="623"]unwomentakwimu

Takwimu bora zinazonadi hali halisi ya maisha ya wanawake na wanaume, wasicha na wavulana , ni nyezo muhimu kwa ajili ya maendeleo na kuwa na ushahidi halisia kwa ajili ya kuunda sera na kupata suluhu ya kufikia usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake.

Wito huo umetolewa na kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya wanawake UN Women kwenye kongamano la kimataifa la takwimu linalofanyika nchini Afrika ya Kusini. Kitengo hicho kimeongeza kuwa takwimu kama hizo zinatoa mwangaza wa maeneo yaliyopigiwa hatua , kutoa ushahidi wa kipi kinafanikiwa, na kuweka bayana mapengo yaliyopo ili juhudi za kuyaziba zifanyike.

UN Women imesema licha ya juhudi bado asilimia 80 ya viashiria vya malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG’s vinakosa takwimu na ni asilimia 41 tu ya nchi kote duniani zinatoa takwimu za ukatili dhidi ya wanawake mara kwa mara.

Huku asilimia 15 ya nchi ndizo zina sheria inayohimiza ukusanyaji takwimu kuhusu masuala ya jinsia, wakati asilimia 13 pekee ya nchi duniani ndio zinatenga bajeti maalumu kwa ajili ya kukusanya takwimu za masuala ya jinsia.

Photo Credit