Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Yemen awasiliana na Rais Abd Rabbo Mansour Hadi

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Yemen awasiliana na Rais Abd Rabbo Mansour Hadi

Pakua

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed amewasili mjini Aden leo kwa ajili ya mikutano na Rais Abd Rabbo Mansour Hadi ,Waziri Mkuu Ahmed bin Daghr na Waziri Abdel Malik Mekhlafi.  Hii ni baada ya mjumbe huyo maalum kumaliza mikutano na viongozi waandamizi kutoka Serikali ya Saudi Arabia, Oman na Qatar mjini Riyadh, Muscat na Doha wiki iliyopita.

Mkutano wake mjini Aden unalenga haja ya ukomeshaji wa uhasama upya na hatua za haraka kushughulikia hali mbaya ya kibinadamu nchini humo. Bwana Ahmed amesisitiza umuhimu wa ukomeshaji wa uhasama ili kuruhusu upanuzi wa misaada ya kibinadamu na kuweka mazingira mazuri ya mchakato wa amani.

Ameongeza kuwa wanahamasisha vyama kurejesha ukomeshaji wa uhasama wa Aprili 10 mwaka jana na kuchukua hatua za haraka ili kuzuia kuzorota kwa hali ya kiuchumi na kibinadamu.

Baadhi ya masuala aliyojadiliana na Rais Hadi ni mambo muhimu ya kuzingatia mafikiano ya Kuwait  kusaidia kumaliza vita na Yemen kurejea katika hali ya amani na utulivu. Amesema kuwa mkataba wa amani ikiwa ni pamoja na mpango wa usalama na kuundwa kwa serikali ya umoja ndio njia pekee ya kumaliza vita ambayo imesababisha hali ya ugaidi nchini Yemen na kwenye ukanda mzima. Bwana Ahmed amemtaka Rais achukue hatua za haraka kwa kuzingatia mapendezo ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mustakhbali wa nchi yake.

Photo Credit