Skip to main content

Ushirikiano ni muhimu kwa mustakhbali wa Palestina-Mladenov

Ushirikiano ni muhimu kwa mustakhbali wa Palestina-Mladenov

Pakua

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kuhusu amani ya Mashariki ya Kati Nickolay Mladenov amekaribisha kutiwa saini kwa mkataba mpya wa shughuli kati ya Israel na Palestina ikiwemo kamati ya pamoja ya kuboresha upatikanaji wa maji na miundombinu ukanda wa Gaza na ukingo wa magharibi wa mto Jordan.

Kwenye taarifa aliyoitoa Bwana Mladenov ameongeza kuwa mkataba huu pamoja na mikataba ya awali kwa ajili ya umeme, maji, mtandao na simu za rununu inazingatia mapendekezo ya chombo cha pande tatu cha kusaka amani ya Mashariki ya Kati Quartet. Amesema ikiwa inatekelezwa kikamilifu, hatua hii itakuwa muhimu kwa kuelekea kupatikana ufumbuzi wa kuwa na mataifa mawili. Ametoa wito kwa pande hizo mbili kufanya ushirikiano ili kuleta suluhu ya mustakhbali wa Palestina.

Photo Credit
UN Photo/JC McIlwaine