Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP na Ubelgiji waungana kusaidia wapalestina

WFP na Ubelgiji waungana kusaidia wapalestina

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP leo limekaribisha mchango wa Euro milioni moja kutoka Ubelgiji ili kusaidia wapalestina 180,000 walio kwenye mazingira magumu huko ukanda wa Gaza na ukingo wa magharibi wa mto Jordan.

Mwakilishi mkazi wa WFP huko Palestina, Daniela Owen amesema fedha hizo zitasaidia kuboresha lishe kupitia mgao wa chakula wa kila mwezi na pia kujaza vocha za kununulia chakula.

Halikadhalika zitatumika kutoa mafunzo kuhusu lishe kwa wanawake wajawazito na wale wanaonyonyesha.

WFP imesema wanufaika ni pamoja na watu 30,000 wa jamii za kibedui zinazohamahama na zile za ufugaji kwenye moja ya eneo linalokaliwa na Israel.

Bi. Owen amesema msaada huo kupitia ushirikiano kati ya WFP na Ubelgiji umeleta tofauti kubwa katika maisha ya watu na kuongeza ustahimili wao wa kukabiliana ugumu wa maisha ya kijamii na kiuchumi.

Zaidi ya asilimia 27 ya wakazi wa Palestina wanakabiliwa na uhaba wa chakula.

Photo Credit
Picha: WFP/Eman Mohammed