Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majadiliano ya kusaka suluhu Cyprus yaanza Geneva

Majadiliano ya kusaka suluhu Cyprus yaanza Geneva

Pakua

Mazungumzo ya kusaka suluhu ya mgogoro wa Cyprus yameanza mjini Geneva Uswisi, viongozi wawili wamekutana chini ya uratibu wa Umoja wa Mataifa, mazungumzo hayo yanatarajiwa kuendelea hadi Januari 11.

Katika mkutano na wandishi wa habari mjini Geneva, mshauri maalum wa Katibu Mkuu kuhusu Cyprus Espen Eide amesema viongozi wa Ugiriki na Uturuki pamoja na ujumbe wao wamekutana hii leo katika mazungumzo yenye tija, ambapo Januari 12 mkutano wa kimataifa kuhusu utatuzio wa mgogoro huo unatarajiwa.

Amesema nchi wadhamini kama vile Ugiriki, Uturiki na Uingereza , Jumuiya ya Ulaya EU, anmbayo ina jukumu maalum la uangalizi pamojaa na ujumbe wa Cyprus ambapo watasaka suluhu kuhusu masuala ya kisualama.

Bwana Eide amesema mchakato mzima sio mrahisi lakini ana matumaini.

(Sautu Eide)

‘‘Inawezekana pia kwasababu sifahamu suala lolote katika majadiliano haya ambalo kwa hakika haliwezi kusuluhishwa, ikiwa kuna utashi toshelevu. Napenda kusisitiza kwamba ubora wa mkutano wa Januari 12 unategemea majadilianao ya Januari 9 na 11.’’

Photo Credit
Espen Barth Eide(kati kati) Nicos Anastasiades kushoto na Mustafa Akinci.(Picha:Maktaba/UNFICYP)