Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama launga mkono harakati za kibinadamu huko Mosul

Baraza la Usalama launga mkono harakati za kibinadamu huko Mosul

Pakua

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limeunga mkono jitihada za Umoja wa Mataifa na wadau wake chini ya uratibu wa serikali ya Iraq, za kufikisha misaada ya kibinadamu kwenye mji wa Mosul na viunga vyake, nchini Iraq.

Rais wa baraza hilo kwa mwezi huu wa Januari Balozi Olof Skoog wa Sweden amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha faragha kilichofanyika kuangazia hali ilivyo nchini Iraq.

(Sauti ya Balozi Olof)

“Wanachama wamekaribisha kitendo kwamba jeshi la Iraq kuchukua hatua kulinda raia wakati wa kampeni ya kijeshi. Halikadhalika wameelezea hofu yao kubwa kuwa raia zaidi ya milioni moja bado hawajifikiwa na misaada ya kibinadamu na kwamba wako kwenye maeneo yaliyo chini ya ISIL au Da’esh huko Mosul na wanakabiliwa na ghasia na ukatili.”

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, idadi ya waliokimbia makwao huko Mosul kutokana na kampeni ya kijeshi iliyoanza tarehe 17 mwezi Oktoba mwaka jana inakaribia 132,000.

Miongoni mwao hao 114,000 wako kwenye maeneo ya dharura.

Photo Credit
Rais wa baraza hilo kwa mwezi huu wa Januari Balozi Olof Skoog wa Sweden.(Picha:UM/Eskinder Debebe)