Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kukatwa kwa bomba kuu la maji Damascus, kwakosesha maji mamilioni ya watu

Kukatwa kwa bomba kuu la maji Damascus, kwakosesha maji mamilioni ya watu

Pakua

Umoja wa Mataifa ina wasiwasi kwamba wakazi takriban milioni nne katika mji mkuu wa Syria, Damascus na maeneo ya jirani hawana maji tangu Desemba 22 baada ya bomba kuu la kusambaza maji kukatwa .

Taarifa ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa misaada ya kibinadamu OCHA inaeleza kuwa vyanzo vikuu viwili vya maji safi ya kunywa vya Wadi barada na Ain-el-Fijah kwa asilimia 70 ya wakazi hao, havifanyi kazi kutokana na kulengwa na miundombinu kuharibiwa.

Licha ya serikali na mamlaka za maji kuanzisha mpango wa usambazaji maji ili kushughulikia uhaba kwa wakazi wa mji huo lakini ni karibu juma moja watu hawajapata maji katika nyumba zao na inawabidi kununua maji kutoka kwa wachuuzi binafsi, ambako hakuna udhibiti wa bei na ubora wa maji.

Umoja wa Mataifa inasema kuwa ukosefu huu wa maji unaweza kusababisha magonjwa yanayotokana na maji, hasa miongoni mwa watoto pia huathiri familia nyimgi kifedha

Watu karibu milioni 15 nchini Syria wanahitaji msaada wa maji na na raia wanatumia asilimia 25 ya mapato yao ili kukidhi mahitaji yao ya kila siku ya maji.

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa pande zote kufikia makubaliano ya amani ili kupunguza mateso ya raia, na kwamba huduma za msingi muhimu kwa maisha, kama vile maji safi ni lazima kulindwa wakati wote.

Photo Credit
Picha: UNICEF