Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMIL sasa kusalia Liberia hadi Machi 2018

UNMIL sasa kusalia Liberia hadi Machi 2018

Pakua

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limeongeza muda wa ujumbe wake huko Liberia, UNMIL hadi tarehe 30 Machi mwaka 2018.

Kuongezwa kwa muda huo uliokuwa umalizike tarehe tarehe 31 mwezi huu, unafuatia azimio lililopitishwa na baraza hilo kwa kura 12, huku wajumbe watatu ambao ni Urusi, Ufaransa na Uingereza wakipinga.

Msingi wa azimio hilo ni pamoja na uwezekano wa kuwepo kwa changamoto kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka 2017 sambamba na kusaidia serikali ya Liberia kwenye mchakato wa maandalizi na kufanyika kwa uchaguzi.

Hivyo azimio linapatia UNMIL mamlaka kadhaa ikiwemo ulinzi wa raia dhidi ya ghasia, kusaidia serikali ya Liberia katika kufuatilia na usimamzi wa haki za binadamu.

Hata hivyo azimio linataka kupunguzwa kwa ukubwa wa kikosi cha askari kutoka 1,230 hadi 434 huku polisi nao wapunguzwe hadi kutoka 606 hadi 310.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametakiwa kuwasilisha ripoti ya hali ilivyo kabla ya tarehe 15 mwezi ujao mwakani.

Photo Credit
Mlinda amani mwanamke wa UNMIL.(Picha:UM/Christopher Herwig)