Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfuko wa dola bilioni 1 wazinduliwa kuchagiza nishati salama

Mfuko wa dola bilioni 1 wazinduliwa kuchagiza nishati salama

Pakua

Tovuti inayofuatilia hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, imetangaza kuwa Bill Gates amezindua mfuko wa dola bilioni Moja kwa ajili ya kusaidia nishati salama zinazobuniwa kwa lengo la kupunguza utoaji wa gesi chafuzi.

Climateaction ambayo inaungwa mkono na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP imesema mfuko huo unaleta pamoja zaidi ya viongozi 20 wenye ushawishi katika ujasiriamali na biashara.

Gates amesema lengo lao ni kujenga kampuni ambazo zitasaidia kuibua teknolojia za kisasa zaidi kwenye sekta ya nishati salama na yenye gharama nafuu.

Mfuko huo utakaodumu kwa miaka 20 utatoa fursa kwa tafiti na kusaidia kampuni changa kupata mitaji na zile ambazo tayari ziko kwenye utendaji ziweze kuboresha shughuli zao za kijasiriamali kwenye sekta ya nishati salama na endelevu.

Photo Credit
Moja ya malighafi za nishati salama nchini Uganda. (Picha:Idhaa ya Kiswahili/John Kibego.)