Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Simamia haki ya mwenzio leo

Simamia haki ya mwenzio leo

Pakua

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu leo hii, Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa amesema kuimarisha haki za binadamu ni kwa ajili ya maslahi ya wote, utulivu kwa kila jamii na maelewano katika ulimwengu wetu ulioshikamana na kila mmoja anajukumu hilo na uwezo huo.

Amesema kampeni mpya ya kimataifa ya "simama kwa ajili ya haki ya mtu leo" iliyoanzishwa na Ofisi ya Haki za Binadamu, inahamasisha watu wote, popote pale walipo, iwe ni katika vitongoji vyao, shuleni, kwenye mitandao ya kijamii, kazini na majumbani mwao kuchangia katika haki za kila mmoja aliyekaribu yake leo, kesho na kila siku.
Amekumbusha kwamba utambuzi wa haki sawa kwa watu wote ulimwenguni ndio msingi wa uhuru, haki na amani duniani,  hususan wakati huu ambapo migogoro yenye kuzidisha mahitaji ya kibinadamu, na kuongeza hotuba zenye chuki kwa wahamiaji na wakimbizi yanazidi kuongezeka.
Na kwa mantiki hiyo ametoa wito kwa serikali kuimarisha haki za binadamu na kwa nchi wanachama na mashirika yote duniani kuimarisha mwitikio wa dhuluma, na kuongeza juhudi zaidi katika kuzuia ukiukwaji wa haki za binadamu.

Photo Credit
Picha:UNRIC