Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres kuapa muda mfupi ujao kuwa Katibu mkuu wa 9:UM

Guterres kuapa muda mfupi ujao kuwa Katibu mkuu wa 9:UM

Pakua

Natts…..

Katibu Mkuu mteule wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akitanabaisha kilichomchagiza kuwania kiti ambacho muda mfupi ujao kitahalalishwa rasmi kuwa chake na kuanza kukikalia kuanzia Januari Mosi 2017 akiwa Katibu Mkuu wa 9 wa Umoja wa Mataifa.

(PHOTO SLIDE)

Ataapishwa punde katika hafla maalumu inayofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York na kuanza kutekeleza safari ndefu ya kuzitumikia nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa lakini kikubwa zaidi ni kutekeleza ahadi alizozitoa wakati wa mchakato wa kuwania kiti hicho ambako alikiri changamoto ni nyingi

(GUTERRES CUT 1)

"Changamoto kubwa kwa hivi sasa ni kuhakikisha tunakuwa na ufanisi zaidi katika diplomasia kwa ajili ya amani, lakini kuna changamoto kubwa za kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko kwenye shirika hili ilikulifanya liwe na ufanisi zaidi, liweze kutimiza ahjadi zaidi kwa watu tunaowatumikia kote duniani. Pia kuna changamoto za kuhakikisha kuwa mafanikio yote yaliyowezekana hivi karibuni , shukrani kwa Katibu Mkuu Ban Ki-moon kama ajenda yam waka 2030 na mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi , kuhakikisha kwamba mikataba hiyo ya kihistoria inatekelezwa. Na ufuatiliaje wake nao pia unatoa changamoto kubwa . Pia masuala yote ya kuhakikisha kwamba haki za binadamu yanachukuliwa kuwa ni jukumu la pamoja la binadamu wote nan chi wanachama.”

Guterres raia wa Ureno, aliyeibuka kidedea miongoni mwa wagombea 14, ameahidi pia kushikia bango masuala ya uwezeshaji wa wanawake, kutafuta ufumbuzi wa mizizi ya migogoro ya muda mrefu, kudumisha hali za watoto , kuchagiza utokomezaji wa umasikini , suluhu kwa wakimbizi na wahamiaji na kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama.

Anaingia madarakani baada ya Katibu Mkuu wa sasa Ban Ki-moon kutoka Korea Kusini kufunga pazia la muhula wake wa miaka 10 hapo Desemba 31.

Natts…..

Photo Credit
Katibu Mkuu mteule Antonio Guterres; picha na UM/ Manuel Elias