Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bokova alaani mauaji ya wana habari Finland

Bokova alaani mauaji ya wana habari Finland

Pakua

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, Irina Bokova, amelaani mauaji ya wana habari Katri Ikävalko na Anne Vihavainen nchini Finland.

Taarifa ya UNESCO imemnukuu Bokova pia akilaani mauaji ya pamoja na ya kiongozi mteule Tiina Wilen-Jäppinen ambayo yalifanyika tarehe nne mwezi huu katika mji wa Imatra, kusini-mashariki mwa Finland nchi ambayo amesema ilikuwa mwenyeji ya maadhimisho ya mwaka huu ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.

Hata hivyo amekaribisha hatua za haraka na mamlaka katika uchunguzi wa uhalifu huo aliosema ni wa kutisha.

Photo Credit
Picha: UNESCO