Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi zadi zahitajika kukomesha ukatili dhidi ya wanawake: Phumzile

Juhudi zadi zahitajika kukomesha ukatili dhidi ya wanawake: Phumzile

Pakua

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la wanawake Phumzile Mlambo-Ngcuka amesema ukomeshaji ukatili dhidi ya wanawake unahitaji kuchochewa zaidi kwa kuongeza kinga na huduma mujarabu zinazohitaji fedha .

Ametoa wito huo wakati wa hafla ya miaka 20 ya juhudi za kukomesha ukatili dhidi ya wanawake iliyoandaliwa na mfuko wa Umoja wa Mataifa katika juhudi hizo au UN Trust Fund, hafla ambayo pia imehudhuriwa na balozi mwema wa UN Women Nicole Kidman ambaye pia ni mchezaji wa filamu.

Bi Phumzile ametambua hjuhudi kubwa zinazofanywa dhidi ya ukatii kwa wanawake na wasichana ambao sasa umekuwa ni mjadala wa hadharani ikilinganishwa na hapo awali hatua iliyoleta mafanikio makubwa katika sheria na juhudi za kushughulikia suala hilo.

Hafla hiyo pia imetumika kukabidhi tuzo mlezi wa taaasisi ya UN Trust Fund Bi Ban Soon-taek kwa jitihada zake za kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.

Photo Credit
UN Photo/Devra Berkowitz