Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP22: Tanzania yaendelea kutekeleza miradi ya kuhimili tabianchi- Makamba

COP22: Tanzania yaendelea kutekeleza miradi ya kuhimili tabianchi- Makamba

Pakua

Tanzania imesema miradi ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi inaendelea kutekelezwa nchini  humo licha ya  kusuasua kwa uchangiaji wa fedha kutoka nchi zinazoongoza kwa utoaji wa hewa chafuzi duniani.

Waziri wa mazingira nchini humo January Makamba amesema hayo akihojiwa na Idhaa hii kutoka Marrakesh, Morocco anakoshiriki mkutano wa COP22, akitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na..

(Sauti ya Makamba-1)

Amesema Tanzania inahitaji dola bilioni 60 kugharimia miradi hiyo lakini...

(Sauti ya Makamba-2)

Amesema suala hilo la uchangiaji wa fedha kwenye miradi ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi litapatia kipaumbele kwenye mjadala utakaofanyika hii leo huko Marrakesh.