Mzozo kati ya Equitorial Guinea na Gabon juu ya mpaka wamalizika

Mzozo kati ya Equitorial Guinea na Gabon juu ya mpaka wamalizika

Pakua

Usuluhishi wa Umoja wa Mataifa kwenye mzozo wa mpaka kati ya Equitorial Guinea na Gabon umehitimishwa leo huko Marrakesh, Morocco kwa viongozi wa nchi mbili hizo kutia saini makubaliano maalum ya kumaliza mzozo huo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alikuwa mwenyeji wa hafla hiyo iliyofanyika kando mwa mkutano wa 22 wa mkutano wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP22.

Usuluhishi ulianza mwaka 2008 kwa mzozo huo kuwasilishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya haki, ambapo hii leo Ban amenukuliwa na msemaji wake akipongeza viongozi wa nchi mbili hizo kwa uongozi wa kisiasa walioonyesha na kufanikisha makubaliano yaliyofikiwa.

Ban amesema hitimisho la mzozo huo wa muda mrefu ni mfano kwa nchi nyingine kuwa changamoto kama hizo zinaweza kusuluhishwa kwa amani.

Nchi mbili hizo zimekuwa zinazozania mpaka kwenye eneo la Mbanié, Cocotiers na visiwa vya Conga tangu miaka ya 1970.

Photo Credit
ICJ