Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwekeza kwa wakulima kutasaidia mabadiliko ya tabinchi.

Kuwekeza kwa wakulima kutasaidia mabadiliko ya tabinchi.

Pakua

Ripoti mpya ya shirika la mfuko wa maendeleo ya kilimo IFAD inaonyesha kuwa kwa kila dola moja inayowekezwa katika mpango wa usaidizi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa wakulima wadogo wadogo ASAP, una manufaa makubwa.

Kwa mujibu wa IFAD inayohudhuria mkutano wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi mjini COP22 mjini Marrakech Morocco, faida hiyo yaweza kuwa kiasi cha dola za kimarekani 1.40 na 2.60 kwa kila dola inayowekezwa, kwa zaidi ya miaka 20 ya kutekeleza makabiliano hayo.

IFAD inaamini kuwa kuwekeza kwa wakulima wadogo wadogo kutasaidia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabainchi kutokana na umuhimu wa kundi hilo katika kilimo.

Photo Credit
UN Photo/Milton Grant