Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yahitaji fedha zaidi kuendelea kusaidia Haiti

WFP yahitaji fedha zaidi kuendelea kusaidia Haiti

Pakua

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema mwezi mmoja tangu kimbunga Matthew kipige Haiti na kuleta madhara makubwa, limepatia misaada ya vyakula takribani wakazi Laki Nne nchini humo.

Mwakilishi wa WFP nchini Haiti, Ronald Tran Ba Huy amesema wanafanya kila wawezalo kufikia wahanga ili wasihaulike wakati huu ambapo wanahitaji dola Milioni 58 kukidhi dharura za mahitaji ya chakula na vifaa.

Amesema wanatumia akiba ya chakula iliyokuwemo nchini humo kusaidia wakazi wa eneo la Jeremie, huku akisema kwa ujumla hadi sasa watu 140,000 wanaishi kwenye makazi ya muda.

Hata hivyo amesema ili kutosheleza mahitaji kwa miezi miwili au mitatu ijayo watahitaji kiasi kingine cha dola Milioni 40 ili kuendeleza usaidizi.

Photo Credit
Uwasilishji wa misaada nchini Haiti.(Picha:UN/MINUSTAH/Nektarios )