Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba wa Paris uzingatie haki za binadamu: Zeid

Mkataba wa Paris uzingatie haki za binadamu: Zeid

Pakua

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein amesema kuanza kutekelezwa kwa mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi hapo kesho kwende sanjari na haki za makundi yaliyoathiriwa na mabadiliko hayo.

Katika taarifa yake kuhusu mkataba huo, Zeid amesema makundi athirika lazima yalindwe, na kusisitiza kuwa nchi lazima zihakikishe hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kama vile miradi ya nishati na maji iwalinde walengwa na sio kuwaathiri.

Kamishna Zeid ameonya kuwa janga la mabadiliko ya tabianchi ni tishio kubwa katika utekelezaji wa ajenda ya maendeleo ya 2030, na kwamba uratibu wa jumuiya ya kimataifa unahitajika ili kuheshimu haki za binadamu hususani katika kupunguza hewa chafuzi.

Ametaka pande wawakilishi watakaohudhurai mkutano wa COP22 wa mabadilio ya tabianchi mjini Marrakech, Morocco kuhakikisha kuwa nchi zinachukua hatua kwa kuzingatia haki za binadamu.

Photo Credit
UN Photo/Mark Garten)