IPU: hatua za kisheria kunyamazisha wabunge zinatia hofu

IPU: hatua za kisheria kunyamazisha wabunge zinatia hofu

Pakua

Muungano wa mabunge IPU, leo Alhamisi umezungumzia ongezeko la kiwango cha ulipizaji kisasi dhidi ya wabunge wanaotumia uhuru wao wa kujileleza kote duniani.

Katika mlolongo wa maamuzi yaliyopitishwa kuhusu haki za binadamu za wabunge , IPU imesisitiza kuhusu ongezeko la hatua za kisheria mahakani na kutimuliwa kwa wabunge katika uwanja wa kisiasa kama njia ya kunyamazisha wapinzani wa kisiasa.

Imeongeza kuwa badala ya kuwasikiliza wapinzani mfumo wa kisheria ndio umekuwa nyenzo ya kuwatupa nje.

Mabunge wanachama wa IPU wameshughulikia kesi za wabunge 129 katika nchi 8 duniani ambao haki zao za binadamu zinadaiwa kukiukwa.

Nyingi ya kesi hizo ni za wabunge kuelezea maoni yao ambayo sio tuu yanawafanya washindwe kutekeleza

Photo Credit
Muungano wa mabunge. (Picha: IPU-log)