Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mgogoro Yemen wazidisha viwango vya njaa na utapiamlo: WFP

Mgogoro Yemen wazidisha viwango vya njaa na utapiamlo: WFP

Pakua

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, lina wasi wasi juu upungufu wa chakula nchini Yemen ambao umeongezaea viwango vya utapiamlo miongoni mwa watoto, hususan kwenye maeneo yenye mzozo.

Mkurugenzi wa WFP anayehusika pia na kanda ya Mashariki ya Kati Muhannad Hadi amesema kuendelea kwa vita nchini Yemen kumeleta mazingira magumu na kuathiri watu wengi hasa wanawake na watoto.

Amesema ziara yao nchini humo imewezesha kushuhudia ongezeko la njaa ambapo inakisiwa mamilioni ya watu hawawezi kuishi bila msaada kutoka nje.

Mathalani walitembelea hospitali, vituo vya lishe na vya afya na kuona matukio mengi ya watoto wenye utapiamlo wakiwasili kutoka maeneo ya vijijini hivyo amesema wanahitaji zaidi ya dola Milioni 257 ili kutoa msaada wa chakula muhimu hadi Machi 2017.

Wakati huo huo ameshukuru wahisani muhimu wa WFP ambao wamechangia kusaidia watu wa Yemen, ikiwa ni pamoja na Marekani, Ujerumani, Japan na Umoja wa Ulaya.

Photo Credit
Mtoto Ahmed mwenye umri wa miaka mitatu apokea matibabu dhidi ya utapiamlo.(Picha:WFP/Abeer Etefa)