Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikao cha 65 cha kamati dhidi ya ubaguzi kwa wanawake chaanza

Kikao cha 65 cha kamati dhidi ya ubaguzi kwa wanawake chaanza

Pakua

Kikao cha 65 cha kamati ya Umoja wa Mataifa ya kupinga ubaguzi dhidi ya wanawake kimeanza leo mjini Geneva, Uswisi kikijadili tarifa zilizowasilishwa na vyama vya kiraia kwenye kamati hiyo kutokaCanada, Burundi, Bhutan na Belarus.

Mada zinahusu utekelezaji wa mikataba ya kutokomeza aina zo zote za ubaguzi dhidi ya wanawake. Masuala ya kukosekana kwa usawa kati ya wanaume na wanawake katika kazi na wingi wa wanawake kutoka jamii ya asili ya Aboriginal katika magereza ni miongoni ya mambo yaliyotajwa huko nchini Canada. Japokuwa taifa hilo lina mikakati ya kupunguza umaskini lakini haijazingatia mwelekeo na tatizo la jinsia.

Washiriki wamependekeza kwa serikali ya Canada iendeleze mikakati ya usawa na kuwapatia wanawake waki-aborigini kipaumbele.

Nchini Burundi taarifa inasema haki za ardhi kutokana hasa na sheria za kimila hazipewi kipaumbele na wanaharakati wamesema bado wanaohodhi ardhi ni wanaume na wamependekeza kupitishwa kwa sheria mpya za urithi ili kuwawezesha wanawake kumiliki ardhi.

Na nchini Bhutan ijapokuwa imepata mafanikio makubwa katika sheria bado kuna mapengo katika suala la utekelezaji na suala la utoaji mimba kwa akina mama .Wakati Belarus imesontwa kidole kwa kukosoa hali ya ukatili dhidi ya wanawake kushiriki katika nyanja za kijamii na kisiasa. Ikiwa pia na kubaguliwa kwa wanawake waislamu na Waroma.

Pia imeshutumiwa kwa kuwepo na pengo la mishahara kati ya wanaume na wanawake na ubaguzi dhidi yawatu wa mapenzi ya jinsia moja (LGBT). Mazungumzo zaidi bado yanajadiliwa na kamati hiyo itatoa mapendekezo yake.

Photo Credit
Mwanamke nchini Burundi akifinyanga udongo kwa ajili ya kuumba nyungu.(Picha:UM//Mario Rizzolio)