Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi ya 1,000 waliokokosa hewa safi Iraq wapata matibabu : WHO

Watu zaidi ya 1,000 waliokokosa hewa safi Iraq wapata matibabu : WHO

Pakua

Shirika la afya ulimwenguni WHO na idara ya afya ya mamlaka ya Ninewa nchini Iraq wanatoa matibabu ya haraka kwa zaidi ya watu 1,000 waliokosa hewa safi nakushindwa kupua katika mkoa wa Qayarra, Ijhala, tarehe 23 Oktoba.

Hii imesababishwa na kuendelea kwa uchomaji wa sulfur katika kiwanda cha Mishraq, kaskazini mwa wilaya ya Qayarra katika jimbo la Ninewa. Mwakilishi wa WHO nchini Iraq Altaf Musani amesema wana wasi wasi kuhusu usalama wa watu katika mkoa wa Qayarra na wamependekeza kwa wale wanaotoa huduma ikiwa ni pamoja na polisi na wauguzi kutumia vifaa vya kujikinga.

Ameongeza kuwa wakishirikiana na mamlaka wanakabiliana na tishio hilo kwa mazingira na wanatoa huduma zinazohitajika za afya kuondoa hatari zaidi. Kuhusu tishio kwa mazingira na ukosefu wa upatikanaji wa vifaa binafsi vya kupumulia vilivyo na hewa ya oksijeni, WHO imewashauri watu kuepuka kuvuta moshi na kutafuta huduma ya afya mara moja kama hawajisiki vyema.

Photo Credit