Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Azimio kuhusu Syria lapitishwa Geneva

Azimio kuhusu Syria lapitishwa Geneva

Pakua

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio ambalo pamoja na mambo mengine linaunga mkono juhudi zozote za dhati za kuiamarisha hali ya kibinadamu huko Aleppo nchini Syria.

Azimio hilo limepitishwa kwa kura 24 huku Saba zikipinga na wajumbe 16 hawakuonyesha msimamo wowote.

Nchi zilizopinga ni pamoja na Urusi, Burundi na China huku Afrika Kusini haikuonyesha msimamo wowote.

Halikadhalika, azimio hilo linakaribisha uamuzi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kuanzisha bodi ya umoja huo ya kuchunguza tukio la kushambuliwa kwa msafara wa misaada ya kibanadamu mwezi uliopita huko Urum al-Kubra.

Wajumbe pia kupitia azimio hilo wametaka Tume ya uchunguzi kuhusu Syria iunge mkono hatua za kusaka wahusika wa tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu Syria wanawajibishwa na ripoti yao iwasilishwe mbele ya baraza hilo ndani ya kikao chake cha 34.

Azimio hilo lilipitishwa baada ya mkutano maalum kuhusu kuzorota kwa hali ya kibinadamu Syria na hali ilivyo huko Aleppo.

Photo Credit
Ripoti ya ukiukwaji wa haki za binadamu Aleppo kusini. Picha: UM/Video capture