ICC yaidhinisha mpango wa fidia ya ishara kwa wahanga wa kesi ya Lubanga

ICC yaidhinisha mpango wa fidia ya ishara kwa wahanga wa kesi ya Lubanga

Pakua

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC iliyoko The Hague Uholanzi, leo imepitisha na kutoa idhini ya kuanza kwa utekelezaji wa mpango uliowasilishwa na mfuko maalumu kwa ajili ya wahanga wanaohusiana na kesi ya Thomas Lubanga Dyilo (TFV). Mpango huo ni wa ulipaji fidia ya pamoja kwa njia ya ishara.

Lubanga alikutwa na hatia ya uhalifu wa kivita wa kuajiri na kutumia watoto wa chini ya umri wa miaka 15 vitani huko Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. TFV imeamriwa kuwasilisha ripoti kila baada ya miezi mitatu.

Mahakama hiyo imekubaliana na mfuko wa TFV kwamba utekelezaji wa ishara wa ulipaji fidia utafungua njia ya kukubali malipo ya fidia katika jamii zilizoathirika. Na mahakama itatoa uamuzi wa fidia isiyo ya ishara muda si mrefu.

Mahakama imesema fidiaa ya ishara itaweka mazingira bora ya kuwafanya waathirika wengi kupata ujasiri wa kujitokeza na kushiriki kwa hiyari huduma zilizotokana na fidia ya pamoja bila hofu ya heshima au usalama wao. Lubanga alikutwa na hatia ya uhalifu wa vita 14 Machi 2014 kwa kuajiri na kutumia watoto wa chini ya umri wa miaka 15 vitani na kuwashirikisha kikamilifu kwenye uasi kati ya Septemba 2002 na Agosti 2003.

Photo Credit