Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugatuzi ni muhimu katika maendeleo endelevu: Ban

Ugatuzi ni muhimu katika maendeleo endelevu: Ban

Pakua

Wakati mkutano kuhusu makazi na maendeleo endelevu ya mijini (Habitat III), unatarajiwa kuanza hapo Jumatatu ya Oktobaa 17 mjini Quito, mikutano ya awali imeendelea ikiwamo jumuiko la dunia la serikali za mitaa ambapo imeelezwa kuwa viongozi wa serikali za mitaa wana wajibu muhimu katika maendeleo endelevu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban Ki-moon ambaye amehudhuria jumuiko hilo amesema maafisa kama vile magavana na mameya wanakabiliwa na mahitaji ya msingi ya wananchi ambayo ni pamoja na makazi, usafiri, na miundombinu.

Ban amesema viongozi wa serikali za mitaa hufanya uamuzi mgumu katika masuala ya kuyapa kipaumbele kwani wanapaswa kusimamia bajeti huku wakiwajibika kwenye serikali ya kitaifa na wapiga kura wao.

Amesema ugatuzi na ugawanywaji wa madaraka na majukumu kwa mamlaka za mikoa na mitaa ni muhimu katika maendeleo endelevu.

Photo Credit
Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon alipotembelea maeneo ya mji wa Quito kabla ya kuzungumza na wawakilishi wa serikali za mitaa kutoka nchi mbali mbali duniani, (Picha: UN Social Media / Ariel Alexovich)