Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afya ya akili na upatikanaji wa tiba nchini Tanzania

Afya ya akili na upatikanaji wa tiba nchini Tanzania

Pakua

Tarehe saba mwezi Oktoba, kumefanyika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya afya ya akili. Hii ni siku ambayo wadau wa afya wakiratibiwa na shirika la afya ulimwengini WHO wanaitumia kuhamasisha kuhusu ufahamu wa magonjwa hayo, tiba na hata kinga.

Wakati siku hii ikiadhimishwa, WHO inasema kwamba usaidizi wa kisaikolojia kwa watu waliokumbwa na kiwewe au msongo wa mawazo kwa kushuhudia mambo ya kutisha upatiwe umuhimu ili kupunguza wimbi la magonjwa ya akili.

WHO katika takwimu zake za hivi karibuni zaidi, inaonyesha kwamba duniani kote mtu mmoja kati ya watu 10 aliugua ugonjwa wa akili.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe wake wa siku hiyo, ameangazia umuhimu wa upatikanaji wa tiba za magonjwa hayo na akaenda mbali zaidi kwa kutaka utolewaji wa huduma za kisailokolojia kwa manusura wa majanga.

Nchini Tanzania takwimu za wizara ya afya zinaonyesha kuwa mtu mmoja kati ya wanne ana magonjwa ya akili. Je huduma za tiba hususani kisaikolojia zinapatikana? Na uelewa wa watu kuhusu usaidizi wa kisaikolojia ukoje? Tuungane na Martin Nyoni wa redio washirika redio SAUT ya Mwanza Tanzania.

Photo Credit
Muuguzi akizungumza na wagonjwa wenye matatizo ya afya ya akili.(Picha:WHO/Marko Kokic)