Ban azungumzia kuachiliwa huru kwa wasichana 21 wa Chibok

Ban azungumzia kuachiliwa huru kwa wasichana 21 wa Chibok

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha ripoti za kuachiliwa huru kwa watoto wa kike 21 kutoka Chibok waliotekwa nyara zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Taarifa ya msemaji wa Ban imemnukuu akisema kuwa bado anasalia na wasiwasi juu ya wasichana wengine pamoja na wahanga wengine ambao bado wanashikiliwa na kikundi cha kigaidi cha Boko Haram.

Amesihi jamii ya kimataifa iendelee kushirikiana na Nigeria katika jitihada za kusaka watoto hao, sambamba na kutoa usaidizi wa kibinadamu huko Kaskazini-Mashariki mwa Nigeria.

Taarifa hiyo imesema mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu huko Afrika Magharibi anaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine kufanikisha suala hilo.

Photo Credit
Ban Ki-moon amekaribisha ripoti za kuachiliwa huru kwa watoto wa kike 21 kutoka Chibok. Picha: UM/Maktaba