Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kutathimini hali ya kisiasa na usalama maziwa makuu kufanyika Angola

Mkutano kutathimini hali ya kisiasa na usalama maziwa makuu kufanyika Angola

Pakua

Wakuu wa nchi na serikali wanachama wa mchakato wa amani, usalama na ushirikiano kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo DRC na ukanda wa maziwa makuu wanatarajia kukutana Luanda Angola.

Wadau hao watakutana kuanzia Oktoba 26 Oktoba mwaka huu ili kutathimini maendeleo ya kisiasa na usalama katika ukanda wa maziwa makuu.Mkutano huo utatanguliwa na wa mawaziri wa mambo ya nje utakaoanza Oktoba 24.

Mbali ya hatua zilizopigwa mkutano pia utatathimini changamoto katika utekelezaji wa makubaliano ikiwemo yaliyopitishwa na nchi wanachama na washirika wao.

Miongoni mwa mada zitakazotamalaki ni tatizo linaloendelea la vikundi haramu Mashariki mwa DRC , ikiwemo vikosi vya ADF, FDLR na suala la kuwajumuisha katika jamii wapiganaji waliopokonywa silaha.

Mkutano huo pia utaangalia hali katika ukanda mzima ikijumuisha mambo yanayoendelea DRC, Burundi, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR.

Nchi wanachama ni pamoja na Angola, Burundi, CAR, Congo DRC, Jamhuri ya Congo, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda, Sudan, Sudan Kusini, Afrika Kusini na Zambia.

Photo Credit
kundi la waasi la FDLR waliojisalimisha.(Picha ya UM/Sylvain Liechti)