Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Thamini kazi ya walimu"-Siku ya Walimu Duniani

Thamini kazi ya walimu"-Siku ya Walimu Duniani

Pakua

Leo ikiwa ni siku ya walimu duniani, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO) linaangazia maslahi ya walimu sambamba na ajenda ya maendeleo endelevu. UNESCO inasema maadhimisho ya mwaka huu yameangukia ndani ya ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030(SDG's) iliyoafikiwa mwaka mmoja uliopita.

Maudhui ya mwaka huu ni "Thamini Walimu, Boresha Hali zao", yanajumuisha kanuni za msingi kuhusu ustawi wa walimu zilizopitishwa miaka 50 iliyopita kwa ushirikiano baina ya UNESCO na Shirika la Kazi Duniani(ILO), na pia yanamulika lengo nambari nne katika ajenda ya maendeleo ya "Kuhakikisha elimu bora, shirikishi na yenye usawa na inayojenga fursa ya maisha ya kujifunza kwa wote".

UNESCO inasema, mfumo wa ajenda ya 2030 kuhusu elimu unaangazia umuhimu wa walimu katika utoaji wa elimu sawa na bora, na hivyo ili kufikia lengo hilo na chini ya mfumo wenye rasilimali za kutosha, ufanisi unaosimamiwa, ni lazima walimu hao wapate mafunzo ya kutosha, waajiriwe, wapewe motisha, na wawezeshwe.

Ifikapo mwaka 2030, walimu milioni 3.2 watahitajika kufikia lengo la elimu ya msingi kwa wote na milioni 5.1 zaidi kufikia elimu ya chini ya sekondari.

Photo Credit
Mwalimu darasani shule ya msingi ya Ndiaremme B nchini Senegal(Picha:UM/Evan Schneider)