Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mawaziri wa Posta kuzungumza juu ya maendeleo endelevu

Mawaziri wa Posta kuzungumza juu ya maendeleo endelevu

Pakua

Mawaziri wa masuala ya posta kutoka nchi mbali mbali duniani wanatakutana Istanbul, Uturuki kujadili jukumu la posta katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Mawaziri hao wanahudhuria kikao cha 26 cha shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mambo ya posta, UPU wenye kauli mbiu, Kufanikisha maendeleo endelevu, unganisha jamii biashara na maeneo.

Mawaziri hao watawajibika kuchunguza mada kama vile ujumuishaji wa kijamii na kiuchumi, uwezeshaji wa biashara na kuwezesha shughuli za posta kukabiliana na mawasiliano ya kisasa na technolojia.

Mkurugenzi mkuu wa UPU Bishar Hussein amesema kuwa mkutano huo unafanyika wakati muhimu zaidi wa sekta ya posta ambapo kuna maendeleo ya teknolojia yanayoenda sambamba an kubadilika kwa mahitaji ya wateja na mifumo ya uendeshaji biashara.

UPU inasema kuwa kutokana na kuwa na mtandao mpana katika kueneza huduma, takwimu za wateja na imani ya wateja wao, posta imejiweka katika nafasi nzuri ya kuhudumia wateja wake.

Photo Credit
Picha:UPU/ screen capture)