Skip to main content

Serikali zaahidi kulinda mazingira ya bahari:IMO

Serikali zaahidi kulinda mazingira ya bahari:IMO

Pakua

Serikali zimetoa wito wa kuchukuliwa hatua zaidi ili kushughulikia taka zinazotupwa baharini hasa za plastiki na chembechembe zingine za plastiki ambazo ni tishio kubwa kwa viumbe na mazingira ya bahari.

Wito huo umetolewa katika mkutano wa 38 wa nchi zilizotia saini mkataba wa London wa ulinzi wa viumbe na mazingira ya bahari. Nchi hizo zimeelezea hofu yake kuhusu suala hilo la taka na plastiki baharini, lakini pia zimesema hatua zimepigwa na baadhi ya nchi katika kuzuia na kushughulikia tatizo la uchafuzi wa mazingira ya bahari utaokanao na taka za plastiki.

Utupaji wa taka za plastiki kutoka melini umepigwa marufuku chini ya mkataba na sheria za kimataifa za udhibiti wa utupaji taka baharini (MARPOL) na mkataba wa London.

Photo Credit
Taka ufukoni nchini Timor Leste.(Picha:UM/Martine Perret)