Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

India yawa nchi ya 62 kuridhia mkataba wa Paris:

India yawa nchi ya 62 kuridhia mkataba wa Paris:

Pakua

India imekuwa taifa la 62, kuridhia mkataba wa Paris wa mabadiliko yatabia nchi. Akipongeza hatua hiyo ya India kutia saini mkataba Jumapili Oktoba 3 kwenye makao makuu ya Umoja wa mataifa , ambayo pi ni siku ya kimataifa ya kupinga machafuko, Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki-moon amesema

(SAUTI YA BAN)

“Leo serikali ya India imeonyesha mtazamo na uongozi wa kimataifa kwa kujiunga na mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabia nchi. Hatua hii ya kihistoria inazidi kuimarisha mpango endelevu wa India wa ukuaji na maendeleo”

Ili mkataba wa Paris uanze kutekelezwa rasmi unahitaji nchi 55 zinazochangia asilimia 55 ya hewa chafuzi duniani kurudhia mkataba huo. Peter Thomson Rais wa baraza kuu ameshuhudia utiaji saini huo na kusema umefanyika katika siku muafaka

(SAUTI YA THOMSON)

"Hatua hii iliyojaa matumaini na uwajibikaji , imefanyika katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mahatma Ghandhi, hususani kwa kuenzi mtazamo na ujumbe wa Mahatma wa kudumisha utu na mazingira"

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini pia naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson ambaye amemuwakilisha Katibu Mkuu amesema (SAUTI YA JAN ELIASSON)

“Katibu Mkuu anaipongeza na kuishukuru India , na kuzitoilea wito nchi nyingine kukamilisha taratibu za kuridhia mkataba wa Paris. Ni lazima tuanze kuutekeleza mkataba wa Paris haraka iwezekanavyo, kwa ajili ya hatima ya vizazi vijavyo na dunia yetu

image
India yaridhia mkataba wa Paris:Picha na UM
Hadi sasa nchi ambazo zimesharidhia mkataba huo zinachangia jumla ya asilimia 47.79 ya uchafuzi wa hali ya hewa duniani. India pekee inachangia asilimia 4.1 ya hewa chafuzi duniani. Hivyo kuridhia kwale leo mkataba huo kunafanya jumla ya nchi 62 zilizoridhia na ambazo zinachangia jumla ya asilimia 52 ya hewa chafuzi duniani. Balozi wa India kwenye Umoja wa Mataifa Syed Akbaruddin hakusita kuonyesha dhamira ya taifa hilo katika uwanja wa kimataifa

(SAUTI YA BALOZI WA INDIA SYED AKBARUDDIN)

“Mmeshuhudia uridhiaji wa India kwa mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabia nchi. Kumbukumbu ya kuzaliwa ya Mahatma Gandhi na siku ya kimataifa ya kupinga machafuko, imechaguliwa mahsusi na waziri mkuu wa India kwa ajili ya uridhiaji mkataba , ili kusisitiza sera za Ghandhi za mambo ya mazingira endelevu, ambayo ni moja ya wosia wa Ghandhi na utamaduni uliodumishwa India kwa muda mrefu” 

Iliyosalia sasa ni asilimia tatu tu, na ikikiamilika, mkataba utaanza kutekelezwa rasmi siku 30 baada ya idadi inayohitajika kufikia.

Photo Credit
Hafla ya India kuridhia mkataba wa Paris: Picha na UM