Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uholanzi yachangia Euro Milioni 12 kwa mfuko wa mazingira

Uholanzi yachangia Euro Milioni 12 kwa mfuko wa mazingira

Pakua

Serikali ya Uholanzi na shirika la mpango wa mazingira la Umoja w    a Mataifa, UNEP, leo wametia saini mkataba mpya ili kuimarisha ushirikiano kati yao ambapo Uholanzi itatenga Euro milioni 12 kwa ajili ya mfuko wa mazingira kwa mwaka 2016-2017.

Kusainiwa kwa makubaliano hayo kumefanyika kati ya mkurugenzi Mtendaji wa UNEP Erik Solheim, na balozi wa Uholanzi nchini Kenya, Frans Makken.

Bwana Solheim amesema mkataba huo unathibitisha uhusiano mkubwa kati ya Uholanzi na ofisi yake, akisema kuwa Uholanzi kutoa usaidizi huo mkubwa kwa kazi yao na fedha hizo ushahidi tosha.

Tangu mwaka 2012, Uholanzi imekuwa mojawapo ya nchi zinazotoa mchango mkubwa kwa mfuko wa mazingira.

Naye Balozi Frans Makken akasema kuwa nchi yake imekuwa mtetezi mkubwa wa mazingira na kwamba wako tayari kunga mkono shirika hilo na mkurugenzi huyo mtendaji mpya Solheim katika kazi yao ya kulinda sayari na watu wake.

Photo Credit
UN Photo/Evan Schneider