Misaada ya kibinadamu yaingia Syria

Misaada ya kibinadamu yaingia Syria

Pakua

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limefanikiwa kufikisha msaada wa chakula katika miji minne nchini Syria.

Maeneo hayo ya Madaya, Kefraya, Zabadani na Foaa, ikiwa ni mara ya kwanza misaada kuwafikia tangu mwezi Aprili.

Umoja wa Mataifa na shirika la hilal nyekundu la Syria waliweza kufikisha misaada hiyo ya kukidhi mahitaji ya watu 60,000 ambao hawajapata usaidi kwa miezi mitano.

Mkuu wa WFP nchini Syria Jakob Kern amesema wamepeleka malori 45 yaliyojaa chakula cha msaada kama vile mchele, maharage, sukari, chumvi na mbaazi  na vitatosha kwa mwezi mmoja.

Nchini Syria, WFP iniwapatia zaidi ya watu milioni nne kila mwezi, asilimia thelathini ya vyakula ambavyo vinafikishwa kupitia mipaka ya nchi na kwa ndege na barabara kwa sehemu zisizoweza kufikiwa kwa urahisi. 

Photo Credit
Misaada ya kibinadamu ikipokelewa Syria baada ya kuwasilishwa na msafara wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na shirika la hilal nyekundu la Syria, SARC. (Picha:WFP)