Skip to main content

Afrika haihiitaji msaada toka nje, bali usawa katika biashara: Rais wa Ghana

Afrika haihiitaji msaada toka nje, bali usawa katika biashara: Rais wa Ghana

Pakua

Rais John Dramani Mahama wa Ghana amehoji nini kilichoyakumba maadili yaliyoanzisha Umoja wa mataifa. Akizungumza katika mkjadala wa wazi wa baraza kuu Jumatano amesema hivi sasa duniani kote k kuna kuta mpya zinazojengwa ili kuwafungia watu, na hali hii itaendelea kwa muda gani?

Amesema anatambua kuwa kuna rasilimali za kutosha kwa nchi za Afrika kwa kiasi kikubwa hasa katika kilimo na na nguvu kazi ambao ni vijana, lakini bara hilo hailifaidiki ipasavyo. Ametaka vikwazo visivyo vya lazima viondolewe na uhusiano wa kiuchumi uimarishwe miongoni mwa nchi ili kuhakikisha hakuna anayesalia nyuma.

Amesisitiza kuwa vijana wengi Waafrika hawatahitaji kuhatarisha maisha yao kusaka maisha mapya ulaya.

(Sauti ya Mahama Cut 1)

"Afrika haihitaji huruma wala msaada kutoka nje ya nchi. Afrika inachohitaji ni nafasi ya haki kwa biashara duniani miongoni mwa mengi. Kuundwa kwa biashara huria barani Afrika ni jambo la kupongezwa na ni lazima lifanywe kwa haraka ili kuboresha fursa bora za biashara kwa vijana"

Na kwa upande wa nchi yake Ghana amesema

(Sauti ya Mahama-Cut 2)

Sisi mara nyingi tumeitwa nguzo ya Afrika, mfano wa demokrasia barani Afrika. Tumechuka hatua za kijasiri kuleta mageuzi ya miundo mbinu ili kuendeleza uchumi

"Kwa lengo la kufikia pato la taifa asilimia 4.9% mwaka huu na malengo mengine mazuri, huku sarafu ikiwa imara, uwekezaji wa kigeni nao umeongezeka hivyo tuko imara."

Photo Credit
Rais John Dramani Mahama wa Ghana.(Picha:UM/Cia Pak)