Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanadamu atatokomea iwapo hatutahifadhi mazingira

Mwanadamu atatokomea iwapo hatutahifadhi mazingira

Pakua

"Itakuwa ni mwisho wa mwanadamu" ikiwa ulimwengu utashindwa kutatua changamoto za mazingira, hiyo ni kwa mujibu wa Mjumbe wa amani wa umoja wa mataifa na mpigania ulinzi wa mazingira Jane Goodall.

Bi. Goodall, anayejulikana zaidi kwa utaalamu wake wa Sokwe, anawasaidia maelfu ya vijana katika nchi zaidi ya mia moja kufahamu umuhimu wa kutunza mazingira, kwa kupitia programu yake ya Roots and Shoots.

Katika mahojiano na Redio ya Umoja wa Mataifa katika siku ya kuadhimisha amani duniani, Bi. Goodall anaeleza ni kwa nini wakati huu ni mgumu zaidi katika utunzaji wa wanyama na mazingira...

"Sababu haswa ni umasikini unaosababisha watu kukata miti kuishi, lakini pia ni maisha yasiyo endelevu ya nchi zingine duniani, kadri nchi zinavyoendelea kiuchumi kama vile China, mahitaji ya maliasili pia yanapanda juu zaidi, na nimeambiwa kwamba, na nadhani ni kweli, kwamba tunatumia kwa kasi zaidi kuliko asili inavyoweza kuhimili, na tukiendele hivi, sahau"

Photo Credit
UN Photo/Amanda Voisard