Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muziki ni kipenzi changu kambini Kakuma-mkimbizi

Muziki ni kipenzi changu kambini Kakuma-mkimbizi

Pakua

Wakati mkutano wa ngazi ya juu ukitarajiwa kufanyika wiki ijayo katika Umoja wa Mataifa hali ya wakimbizi walioko sehemu mbali mbali duniani iko njia panda huku wakiendelea kukabiliana na changamoto mbali mbali, wengi wakiwa na ndoto kwamba watakuwa na fursa ya kuishi maisha ya baada ya kambini na hata kurejea nyumbani na kuendeleza nchi zao.

Mmoja wa wakimbizi hao ana ndoto ya kupata elimu na kisha kurejea nchi alikotoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC si mwingine bali ni Stephen Mashuka. Je yuko wapi na ana matumaini gani? Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala hii.

Photo Credit
Mkimbizi Stephen akiwa kambini Kakuma nchini Kenya.(Picha:UNHCR/Video capture)