Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bunge lamwondoa madarakani Rais wa Brazil

Bunge lamwondoa madarakani Rais wa Brazil

Pakua

Kufuatia kitendo cha bunge la Brazil kupiga kura kuridhia kushtakiwa kwa rais wa nchi hiyo, Dilma Rousseff, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ametambua hatua hiyo sambamba na ile ya kuapishwa kaimu rais Michel Temer kushika madaraka hayo.

Taarifa ya msemaji wake imemnukuu akimtakia kila la heri Rais Temer anapoanza awamu hiyo ya uongozi akisema ana imani na Brazil chini ya uongozi wake na kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea na udau wa karibu na nchi hiyo.

Ban ametumia fursa hiyo pia kumshukuru Bi. Rousseff kwa ushirikiano na jitihada zake kwenye kazi za Umoja wa Mataifa wakati wa uongozi wake.

Photo Credit
UN Photo/Turkey