Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bangladesh sitisheni hukumu ya kifo dhidi ya kiongozi wa upinzani:UM

Bangladesh sitisheni hukumu ya kifo dhidi ya kiongozi wa upinzani:UM

Pakua

Wataamu hao wamelaani vikali  hatua hiyo na kuitaka serika kumpa nafasi ya kujitetea tena mahakamani. Bwana  Ali alihukumiwa mwaka  2014 katika mahakama ya ICT nchini Bangladesh inayo walenga watuhumiwa wa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu ulio fanywa mwaka 1971 wakati wa vita vya ukombozi wa Bangladesh.

ICT ni mahakama yenye mamlaka ya kuhukumu watuhumiwa wa makosa ya jinai ikiwemo, uhalifu dhidi ya binadamu, mauaji ya kimbari na uhalifu wa kivita. Bw Ali na wenzake 17 walihukumiwa kunyongwa hadi kifo kutokana na uhalifu dhidi ya binadamu uliofanywa wakati wa vita vya ukombozi nchini humo.

Watano kati wa wahukumiwa hao tayari wameshanyongwa. Hukumu ya Kiongozi huyo wa upinzani imeripotiwa kuwa na dosari nyingi kutoka upande wa serikali ya nchi hiyo ambapo UN imeitaka Bangladesh kufuata kanuni za kisheria katika zoezi zima la hukumu hiyo.

Photo Credit