Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zeid aitaka Maldives kurejea msimamo wa awali wa kupinga hukumu ya kifo

Zeid aitaka Maldives kurejea msimamo wa awali wa kupinga hukumu ya kifo

Pakua

Kamisha Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Zeid Ra’ad Al Hussein Jumanne ameitaka serikali ya Maldives kujizuia kutekeleza hukumu za vifo kama ilivyopanga na badala yake kurejesha sheria iliyokuwepo nchini humo tangu mwaka 1954 inayopinga hukumu hiyo.

Zeid amesema, Maldives imekuwa mfano mzuri kwa muda mrefu ikiongoza kimataifa katika juhudi za kukomesha matumizi ya hukumu ya kifo , hivyo ameongeza inasikitisha sana kuona mlolongo wa hatua zimechukuliwa kurejesha hukumu ya kifo nchini humo.

Tangu Novemba mwaka jana kumekuwa na mabadiliko yanayotia hofu kuhusu hukumu ya kifo Maldives , yakimaliza mila ya muda nrefu ya kubadili hukumu ya kifo kuwa kifungo cha maisha , na tarehe 30 Novemba 2015, mahakama kuu nchini humo ikaamua kuwa Rais hana tena mamlaka ya kura ya turufu endapo m aamuzi ya hukumu ya kifo yakitolewa.

Photo Credit
Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein.(Picha: Maktaba/UM/Violaine Martin)