Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vituo vya afya Syria vimeshambuliwa kwa makombora ya angani

Vituo vya afya Syria vimeshambuliwa kwa makombora ya angani

Pakua

Umoja wa Mataifa umeeleza kusikitishwa na uharibifu wa miundombinu ya kiraia unaoendelea nchini Syria, hususan vituo vya afya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya kuratibu masuala ya kibinadamu (OCHA), Umoja wa Mataifa umepokea ripoti za mashambulizi matano ya angani dhidi ya hospitali.

Hospitali tatu zililengwa katika mkoa wa Aleppo mnamo Julai 30, na nyingine mbili kulengwa kwenye mikoa ya Dara’a na Idleb, mnamo Julai 31 na Julai 30 mtawalia.

Halikadhalika, hifadhi ya damu ya Atareb, mkoani Aleppo iliharibiwa mnamo Julai 31. Kumeripotiwa makumi ya wahanga na majeruhi katika mashambulizi hayo, wakiwemo akina mama waja wazito na watoto.

Umoja wa Mataifa unaendelea kutoa wito kwa pande zote kinzani kukomesha uharibifu wa hospitali na miundombinu mingine ya kiraia, na kutimiza wajibu wao chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu nay a haki za binadamu.

Photo Credit