Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katika siku ya urafiki, tudumishe upendo na kuepusha chuki:Ban

Katika siku ya urafiki, tudumishe upendo na kuepusha chuki:Ban

Pakua

Katika siku ya kimataifa ya urafiki, Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema , masuala kama umasikini, ghasia, ukiukaji wa haki za binadamu na matatatizo mengine makubwa katika ajenda ya kimataifa vinakasumba ya kutoheshimu misingi na mila zilizoanzishwa zaidi ya karne iliyopita.

Ban amesema wakati uchoyo unashinda wasiwasi kuhusu afya ya dunia yetu au wakazi wake, wakati misimamo na itikadi ni inatafuatwa kwa gharama zozote, na wakati watu wanateseka kwa ukiukwaji wa haki za binadamu kwa sababu wao wanachukuliwa kwa namna fulani isiyo sawa, urithi wa ubinadamu utasalitiwa na mustakabali wetu ustawi wa dunia kuwekwa hatarini.

Ameongeza kuwa urafiki ni furaha inayoambatana na ustawi wa maisha ya binadamu, na muungano katika furaha hiyo unaweza kuchngia mabadiliko muhimu katika dunia ambayo yanahitajika haraka ili kuwa na utulivu wa kudumu. Amesisitiza kuwa katika kuadhimisha siku hii ya urafiki watu hamasishe na kukumbatia mahusiano mazuri, ili kuboresha maisha yetu na kuwa na mustakhbali mzurui wenye amani na furaha.

Photo Credit
UN Photo/Sophia Paris