Ni mtu mmoja tu kati 100 anayenusuriwa katika biashara haramu ya watu:UNODC
Ni mtu mmoja tu kati ya 100 anayenusuriwa kutoka kwenye biashara haramu ya binadamu , kwa mujibu wa afisa anehusika na mambo ya biashara ya usafirishaji haramu wa binadamu kwenye ofisi ya Umoja wa mataifa ya madawa na uhalifu UNODC.
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kupinga biashara haramu ya binadamu, afisa huyo wa UNODC, Simone Monasebian, amesema wahanga wa biashara haramu ya binadamu ni pamoja na wale wa ndoa za kupangwa, watumwa wa ngono, wa ajira ya watoto, askari watoto n ahata wale ambao viungo vyao vya mwili vinaibiwa.
Bi Monasebian anaelezea nini kinaifanya biashara haramu ya binadamu kuwa ya kifisadi na uhalifu
(SAUTI YA MONASEBIAN)
“Risasi inaweza kutumiwa mara moja tu, msokoto wa cocaine unaweza kutumiwa mara moja, sindano za heroin mtu anaweza kujidunga mara moja tu, lakini mtu anaweza kutumiwa mara chungu nzima kama bidhaa katika biashara haramu ya watu kwa kuwa mfanyakazi mtoto, kisha kuwa mtumwa wa ngono au hata kuchukuliwa viungo vyake vya mwili. Ni biashara yenye faida kubwa, ya mabilioni ya dola.”
Siku ya kimataifa ya kupinga biashara haramu ya binadamu huadhimishwa kila mwaka tarehe 30 Julai.