Natalia Kanem ateuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa UNFPA

Natalia Kanem ateuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa UNFPA

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametangaza leo kuwa amemteua Dkt. Natalia Kanem kutoka Panama, kuwa msaidizi wake na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA).

Dkt. Kanem atamrithi Bi Kate Gilmore wa Australia, ambaye Katibu Mkuu amemshukuru kwa huduma yake ya kujituma kwa Umoja wa Mataifa.

Dkt. Kanem ana uzoefu wa miaka 25 katika nyanya za afya, afya ya uzazi, amani, sheria ya jamii na masuala ya kiutu. Zamani akifanya kazi na Ford Foundation, Dkt. Kanem aliwahi kusimamia miradi iliyomulika masuala ya afya ya uzazi Afrika Magharibi.

Photo Credit
Dkt. Natalia Kanem. Picha:UNFPA